KIMBUNGA CHAUA WATU 27 HUKO VIETNAM

TAREHE 06-11-2017
Kimbunga  Damrey kimepiga maeneo ya kusini na kati ya Vietnam na kusababisha vifo vya watu 27, na wengine zaidi ya 20 hawajulikani waliko.
Kimbunga hicho kilifika maeneo ya bara  kikiwa na upepo unaovuma kwa kasi ya kilomita 90 kwa saa, ambapo Nyumba zaidi ya  elfu arobaini  zimeharibiwa vibaya na maelfu ya watu wamehamishwa makwao, na Maeneo mengi yakiwa hayana umeme.

Hata hivyo Eneo lililoathiriwa zaidi ni jiji la Nha Trang lililopo umbali wa  kilomita  mia tano  kusini mwa jiji la Da Nang, katika pwani ya nchi hiyo ambapo viongozi wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Asia na Pasific (Apec) wanatarajiwa kuhudhuria mkutano mkuu baadaye wiki hii.
KIMBUNGA CHAUA WATU 27 HUKO VIETNAM KIMBUNGA  CHAUA WATU  27 HUKO VIETNAM Reviewed by safina radio on November 06, 2017 Rating: 5

No comments