RAIS MUGABE AMESISITIZA KUWA YEYE NDIE KIONGOZI HALALI WA ZIMBABWE

TAREHE 17-11-2017



Rais Robert Mugabe anasisitiza kuwa yeye ndiye kiongozi halali wa Zimbabwe na hataki kushiriki mazungumzo yanayofanywa na Kasisi mmoja wa Kikatoliki ya kumuezesha rais huyo mwenye umri wa miaka 93 kuondoka madarakani kwa amani baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Habari kutoka kwa  washirika wa ngazi ya juu waliowekwa katika kizuizi cha nyumbani pamoja na Mugabe na mkewe, Grace, nyumbani kwa kiongozi huyo mjini Harare, imesema Mugabe hana mipango ya kujiuzulu kwa hiari kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika  mwaka ujao.

Upinzani nchini humo umemtaka Mugabe ajiuzulu maramoja na kuundwa haraka serikali ya mpito.

Katibu Mkuu wa chama cha MDC-T chake Morgan Tsvangirai amesema wanaunga mkono hatua ya jeshi lakini nchi inapaswa kurejeshwa haraka katika uongozi wa kikatiba.

Wajumbe maalumu waliotumwa na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wanafany amazungumzo kuhusu hatima ya Mugabe na viongozi wa Zimbabwe.


Nao maafisa kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika - SADC wanakutana baadaye leo katika mji mkuu wa Botswana, Gaberone kuijadili hali hiyo.
RAIS MUGABE AMESISITIZA KUWA YEYE NDIE KIONGOZI HALALI WA ZIMBABWE RAIS  MUGABE AMESISITIZA KUWA YEYE NDIE KIONGOZI HALALI WA ZIMBABWE Reviewed by safina radio on November 17, 2017 Rating: 5

No comments