WAZIRI MKUU MH. MAJALIWA AMWAGIZA SIRRO KUWAKAMATA BW. BAHAMAN WA KAMPUNI YA NAS KWA KUTAKA KUTOA MAGARI BANDARINI KWA KUTUMIA JINA LA WAZIRI MKUU
TAREHE 29-11-2017
Waziri mkuu wa
jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassimu Majaliwa amemtaka mkuu wa
jeshi la polisi nchini IGP Saimon Sirro kuwakamata Bw Bahaman wa kampuni NAS na
wakala wa kampuni ya WOMAC SAMWEL kwa kutaka kutoa bandarini magari makubwa
aina ya Semtrella 44 kwa kutumia jina la waziri mkuu.
Mh Majaliwa ametoa
agizo hilo alipofanya ziara ya
kushtukiza katika bandari ya Dar-es-salaam baada ya kupata taarifa za
mfanyabiashara huyo kutaka kutapeli uongozi wa bandari kwa kutak akutoa magari
hayo yaliyoingizwa hapa nchini mwaka 2015 kutoka nchini Uturuki.
Aidha waziri mkuu
ameitaka mamlaka ya usimamizi wa bandari hapa nchini TPA kufanya kazi kwa
mujibu wa sheria na kutowasikiliza wafanyabiashara wanaotaka kukwepa kodi madai
ya kupewa vibali vya msamaha wa kodi kutoka kwa viongozi wa juu serikalini.
Amesema kuwa
serikali ya awamu ya tano imekuwa ikisimamia ukusanyaji wa mapato,hivyo
haitawavumilia wafanyabiashara wanaotumia majina wa viongozi wakubwa hapa
nchini ikiwemo jina la rais kuingiza bidhaa zao bila kulipa mapato ya serikali
kwa maendeleo ya watanzania wote.
Hata hivyo ziara ya
waziri mkuu imekuja siku chache baada ya rais wa jamuhuri ya muungano wa
Tanzania Mh John Magufuli kufanya ziara nyingine ya kushtukiza bandarini hapo
na kugundua kuwepo kwa magari 53 ya
wagonjwa yaliyoingizwa hapa nchini mwaka
wa 2015 bila mmiliki wake kujulikana.
WAZIRI MKUU MH. MAJALIWA AMWAGIZA SIRRO KUWAKAMATA BW. BAHAMAN WA KAMPUNI YA NAS KWA KUTAKA KUTOA MAGARI BANDARINI KWA KUTUMIA JINA LA WAZIRI MKUU
Reviewed by safina radio
on
November 29, 2017
Rating:

No comments