WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU AMEWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NCHINI KUTAMBUA NAFASI ZAO

TAREHE 07-11-2017

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka Maafisa maendeleo ya jamii nchini kutambua nafasi zao katika kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika uchumi wa Viwanda.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo Mjini Dodoma wakati akifungua mkutano wa 12 wa sekta ya maendeleo ya jamii ambapo ameutumia mkutano huo kuwataka maafisa hao wa maendeleo ya jamii kuji tathmini kiutendaji na kufanya mabadiliko ya kiutendaji ili kuamsha ari ya wananchi katika kushiriki uchumi wa viwanda.

Aidha, Waziri Mwalimu amesema kuwa Wizara ilifanya tathmini ya mchango wa sekta ya maendeleo ya jamii kwa miaka hamsini ya Muungano na kubaini kuwa ari ya wananchi ya kuchangia maendeleo kwa sasa imeshuka ikilinganishwa na miaka ya 1960 hadi 1970.


Mbali na hayo ameongeza kuwa mitaala ya vyuo vinavyofundisha taaluma ya maendeleo ya jamii ni lazima itazamwe upya kama inaakisi maendeleo ya karne ya 21 sambamba na kutazama majukumu ya maafisa hao ngazi ya Wilaya na Mkoa kama yanaendana na  matarajio ya serikali ya awamu ya tano.
WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU AMEWATAKA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NCHINI KUTAMBUA NAFASI ZAO WAZIRI  WA AFYA  MH. UMMY MWALIMU  AMEWATAKA  MAAFISA  MAENDELEO  YA  JAMII NCHINI  KUTAMBUA  NAFASI  ZAO Reviewed by safina radio on November 07, 2017 Rating: 5

No comments