IMEELEZWA KUWA CHANZO CHA ONGEZEKO LA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU NI KUKOSA MALEZI BORA YA WAZAZI.

TAREHE 06-11-2017


Imeelezwa kuwa chanzo kimojawapo kinachosababisha ongezeko la watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu hapa nchini ni baada ya  kukosa malezi bora kutoka kwa wazazi wao.

Hayo yameelezwa na afisa ustawi wa jamii wilaya ya Arumeru Bi Restusta Mvungi wakati akizungumza na Redio Safina kuhusu haki mbalimbali za watoto pamoja na athari wanazokutana nazo baada ya wazazi wawili kutengana katika familia.

Amesema kuwa katika shughuli zao za ustawi wa jamii wamebaini kuwa watoto wengi yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu wana matatizo ya kifamilia hasa baada ya wanandoa kutengana,ambapo mbali na kuishi katika mazingira hayo pia wanaathirika kisaikolojia na kujiona hawana thamani katika jamii.

Ameongeza kwamba ili kukabiliana na changamoto hiyo wao kama watu wanaoshughulika na ustawi wa jamii wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuwalea watoto wakati wazazi wakiwa wawili na namna ya kusuhisha matatizo yao pale wanapohitilafiana.


Hata hivyo ofisi za ustawi wa jamii hapa nchini hufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kuwahudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi,haki za watoto pamoja na  watu wenye ulemavu na wazee.
IMEELEZWA KUWA CHANZO CHA ONGEZEKO LA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KWENYE MAZINGIRA MAGUMU NI KUKOSA MALEZI BORA YA WAZAZI. IMEELEZWA   KUWA  CHANZO  CHA  ONGEZEKO  LA  WATOTO  YATIMA NA WANAOISHI  KWENYE  MAZINGIRA  MAGUMU  NI KUKOSA  MALEZI  BORA YA WAZAZI. Reviewed by safina radio on November 06, 2017 Rating: 5

No comments