TAKRIBANI WATU 200 WAFARIKI KATIKA TETEMEKO LA ARDHI HUKO IRAN
TAREHE 13-11-2017
Takriban
watu 200 wameuawa baada ya tetemeko lenye ukubwa wa kipimo cha Richa cha 7.3
lililotokea katika mkoa ulio magharibi mwa Iran wa Kermanshah.
Kulingana
na kituo cha Marekani USGS tetekemo hilo lilitokea umbali wa kilomita 33.9
chini ya ardhi na lilisikika nchini Uturuki, Israel na Kuwait
Wengi
wa waathiriwa walikuwa katika mji wa Sarpol-e Zahab, kilomita 15 kutoka mpakani
na kutoka kilometa 30 kusini magharibi mwa mji wa Halabja karibu na mpaka wa
Iran..
Kwa
mujibu wa afisa wa shirika la msalaba mwekundu nchini Iran, Morteza Salim amesema
kuwa uharibifu umeripotiwa kutokea katika vijiji vinane na baadhi ya vijiji
vimekumbwa na matatizo ya nguvu za umeme na mawasiliano yamevurugwa.
TAKRIBANI WATU 200 WAFARIKI KATIKA TETEMEKO LA ARDHI HUKO IRAN
Reviewed by safina radio
on
November 13, 2017
Rating:

No comments