WAZIRI WA SHERIA PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI AMEKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA SHERIA WA CHINA ZAO DA CHING.

TAREHE 30-11-2017



Waziri wa Katiba na Sheria Profesa. Palamagamba Kabudi amekutana na Naibu waziri wa Sheria wa China Zao Da Ching na kujadili masuala mbalimbali ikiwemo kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na China.

Kikao hicho kati ya Profesa. Kabudi na Naibu Waziri huyo wa Sheria wa China Bw. Ching na ujumbe wake umefanyika jijini Dar es salaam,ambapo Katika kikao hicho Waziri Palamagamba amesema kuwa Tanzania na China itaongeza ushirikiano wake katika maeneo mengine muhimu ikiwemo Ulinzi na Usalama.

Akizungumzia ziara ya Naibu Waziri huyo wa Sheria wa China na ujumbe wake, Profesa,Kabudi amesema kuwa ziara hiyo itafungua milango mipya katika nyanja mbalimbali za maendeleo.


Hata hivyo naibu waziri huyo wa Sheria wa China,Disemba Mosi mwaka huu  atafanya ziara ya siku moja visiwani Zanzibar ambapo atakutana na Jaji Mkuu  wa Jamuhuri  ya Muungano wa Tanzania Profesa. Ibrahim Juma na viongozi wengine wa Zanzibar.
WAZIRI WA SHERIA PROFESA PALAMAGAMBA KABUDI AMEKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA SHERIA WA CHINA ZAO DA CHING. WAZIRI  WA  SHERIA  PROFESA   PALAMAGAMBA  KABUDI  AMEKUTANA  NA NAIBU  WAZIRI  WA  SHERIA  WA  CHINA  ZAO DA CHING. Reviewed by safina radio on November 30, 2017 Rating: 5

No comments