WAHAMIAJI 50 WAKAMATWA KATIKA MTAA WA BUGANDA KATA YA CHIBULA WILAYANI ILEMELA MKOANI MWANZA.
TAREHE 16-11-2017
Operesheni ya
kuwakamata wahamiaji Haramu iliyoanza mwezi Septemba Jijini Mwanza imesaidia
kukamata zaidi ya wahamiaji 50 katika Mtaa wa Buganda Kata ya Chibula Wilayani
Ilemela Mkoani Mwanza wakiwa katika shughuli za kilimo na uvuvi kwenye mwamabao
wa Ziwa Victoria.
Afisa Uhamiaji Mkoa wa
Mwanza Naibu Kamisha Paul Ranga amesema uhamiaji huo haramu umekamatwa Novemba
Mwaka huu baada ya Maofisa Uhamiaji kupewa taarifa za siri na baadhi ya
wananchi.
Aidha, Afisa huyo wa
Uhamiaji wa Mkoa wa Mwanza amesema zoezi hilo la uhakiki wa hati za uhifadhi
kwa wageni 297 imebainika wageni 34 hati zao ni feki.
Kamishna Ranga ameongeza kuwa zaidi ya
Wahamiaji haramu 120 kutoka nchi tisa ikiwemo Burundi, Ethiopia, Kenya
watafikishwa Mahakamani huku wakitaja sababu za Wahamiaji hao kuja Tanzania ni
pamoja na mazingira Magumu nchini kwao.
Vile vile, amesema kuwa
mbali na mazingira kuwa magumu ya nchi wanakotoka wahamiaji hao lakini lengo
kubwa linalowafanya wahamiaji hao haramu kuja Tanzania ni pamoja na kwenda
kuishi Afrika Kusini kutokana na wao kuwasiliana na ndugu zao waliko huko kwa
ajili ya kazi hivyo, Tanzania ni kama njia ya Kufikia.
WAHAMIAJI 50 WAKAMATWA KATIKA MTAA WA BUGANDA KATA YA CHIBULA WILAYANI ILEMELA MKOANI MWANZA.
Reviewed by safina radio
on
November 16, 2017
Rating:

No comments