WAZIRI MKUU WA ISRAEL BENJAMINI NETANYAHU AWAONYA WANAMGAMBO WA GAZA
TAREHE 13-11-2017
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amewaonya wanamgambo wa Gaza dhidi
ya kuishambulia Israel baada ya kundi la jihadi kuapa kulipiza kisasi kutokana
na moja ya mahandaki yake kushambuliwa.
Netanyahu amesema leo kuwa Israel itajibu kwa shambulizi kubwa iwapo mtu
yeyote atajaribu kuishambulia nchi yake.
Waziri Mkuu huyo ameongeza kuwa Israel inalishutumu kundi la Hamas ambalo
linaidhibiti Gaza kuhusika na mashambulizi yaliyoanzishwa kutoka kwenye eneo
hilo.
Kundi hilo limeapa kulipiza kisasi baada ya handaki lake lililochimbwa
kutoka Gaza hadi Israel, kushambuliwa mwezi uliopita na kuwaua baadhi ya
wapiganaji.
Katika matukio kadhaa wapiganaji wa Gaza walifanikiwa kupata taarifa za
siri kutoka Israel kupitia handaki hilo wakati wa mapigano ya mwaka uliopita.
WAZIRI MKUU WA ISRAEL BENJAMINI NETANYAHU AWAONYA WANAMGAMBO WA GAZA
Reviewed by safina radio
on
November 13, 2017
Rating:

No comments