MAMIA YA WAHAMIAJI WAOKOLEWA KATIKA PWANI YA LIBYA

TAREHE 1-11-2017

Mamia ya wahamiaji wameokolewa katika pwani ya Libya,ambapo Maafisa wa polisi nchini humo wamesema kuwa jumla ya wahamiaji 300 wengi wao wakiwa ni kutoka mataifa ya kusini mwa Jangwa la Sahara, wameokolewa jana katika boti mbili na kupelekwa kwenye ufukwe kwa Tripoli ambako walipatiwa matibabu na msaada.

Mlinzi mmoja wa pwani amesema kuwa jumla  ya watoto 15 na wanawake 25 ni miongoni mwa wahamiaji waliookolewa.


 Shirika la Umoja wa Mataifa la Wahamiaji, IOM linakadiria kuwa zaidi ya wahamiaji laki moja  wengi wao wakiwa kutoka Libya, wamevuka bahari na kwenda Italia kwa mwaka huu, huku kiasi ya wahamiaji elfu kumi na nane wakiwa wamezuiwa.
MAMIA YA WAHAMIAJI WAOKOLEWA KATIKA PWANI YA LIBYA MAMIA  YA  WAHAMIAJI  WAOKOLEWA  KATIKA  PWANI YA LIBYA Reviewed by safina radio on November 01, 2017 Rating: 5

No comments