WAZIRI MKUU WA TANZANIA MH. MAJALIWA KASSIM MAJALIWA AELEZA SABABU ZA UPUNGUFU WA WATUMISHI KATIKA SEKTA MBALIMBALI.

TAREHE 16-11-2017

Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassimu Majaliwa amesema kuwa upungufu wa watumishi katika sekta mbalimbali za umma umetokana na zoezi la serikali la kuwaondoa watumishi hewa pamoja na wenye vyeti vya kugushi.

Mh Majaliwa ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya wabunge waliotaka kujua  ni serikali itawaajiri  watendaji wa vijiji na kata hapa nchini ili fedha za miradi zinazopelekwa katika maeneo yao ziweze kusimamiwa vizuri na kutumika kama ilivyopangwa.

Amesema kuwa zoezi la kuwaondoa watumishi hao lilisababisha kutokea kwa upungufu wa rasilimali watu katika sekta mbalimbali ikiwemo afya na elimu lakini kwa sasa serikali imetangaza kuwaajiri watumishi wengine wapya zaidi ya elfu hamsini na mbili watakaojaza nafasi hizo.

Kuhusu upungufu wa watendaji wa mitaa na kata Mh waziri mkuu amesema kuwa kazi ya kuaajiri watendaji hao hufanywa na halmashauri za wilaya kutokana na uhitaji wao na bajeti waliojiwekea ili fedha zinazopaswa kusimamiwa na viongozi hao wa kata na vijiji ziweze kusimaiwa vizuri.


Hata hivyo amesema kuwa azma ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kila sekta hapa nchini inapata watumishi wa kutosha na kwa sasa rais ameshaanza kutoa kibali ajira katika sekta za afya,elimu na jeshi.
WAZIRI MKUU WA TANZANIA MH. MAJALIWA KASSIM MAJALIWA AELEZA SABABU ZA UPUNGUFU WA WATUMISHI KATIKA SEKTA MBALIMBALI. WAZIRI MKUU WA TANZANIA MH. MAJALIWA KASSIM MAJALIWA AELEZA SABABU ZA UPUNGUFU WA WATUMISHI KATIKA SEKTA MBALIMBALI. Reviewed by safina radio on November 16, 2017 Rating: 5

No comments