WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMEWATAKA MAWAZIRI NA MANAIBU MAWAZIRI KUACHA KUTOA MATAMKO YASIYOTEKELEZEKA.
08-11-2017
Waziri Mkuu Kasim
Majaliwa amewataka Mawaziri na Manaibu Mawaziri kujiepusha na utoaji matamko
yasiyotekelezeka ili kuepuka mikanganyiko serikalini.
Waziri Majaliwa ametoa
kauli hiyo wakati akifungua kikao kazi cha baraza la Mawaziri kilichofanyika
katika Ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema
kuwa kabla ya kutoa matamko ni vyema viongozi hao wakajiridhisha iwapo jambo
hilo halitaleta athari kibajeti na kisera na kama lipo katika bajeti za wizara
zao.
Aidha, Mh. Majaliwa
amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya uongozi ili
kithibitishia jamii kuwa wameteuliwa katika nafasi hizo kutokana na uwezo wao
wa utendaji.
Vile vile, Waziri Mkuu
amewataka Mawaziri kujiwekea utaratibu wa kusikiliza hoja na shida za wabunge
na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMEWATAKA MAWAZIRI NA MANAIBU MAWAZIRI KUACHA KUTOA MATAMKO YASIYOTEKELEZEKA.
Reviewed by safina radio
on
November 08, 2017
Rating:

No comments