NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI MH. JUMAA AWESO AMEWATAKA WAHANDISI WA MAJI KATIKA HALMASHAURI ZOTE KUSIMAMIA VYEMA MIRADI YA MAJI.
TAREHE 23-11-2017
Naibu waziri wa maji na
umwagiliaji Mh Jumaa Aweso amewataka waandisi wa maji wa halmashauri zote hapa
nchini kusimamia vyema miradi ya maji pamoja na jumuiya za watumia maji ili
uwekezaji unaofanyika katika sekta hiyo uweze kuleta tija.
Mh Aweso ameyasema hayo
muda mfupi baada ya kuzungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo cha maji
jijini Dar-es-salaam,ambapo amesema kuwa upungufu wa wataalamu wa maji elfu saba unasababisha kusuasua
kwa baadhi ya miradi ya maji hapa nchini.
Amesema kuwa serikali
inazitaka jumuiya zote zinazohusika na masuala ya miradi ya maji, lazima ziwe
zimesajiliwa pamoja na kuwa na mfumo mzuri wa matumizi mazuri ya fedha katika
miradi ya maji na kuepuka ubadhirifu unaoweza kujitokeza.
Naibu waziri huyo
ameongeza kuwa ili kuhakikisha fedha za maji zinazopelekwa katika halmashauri
hizo zinatumika kama ilivyopangwa ni lazima wahandisi wote wa halmashauri hizo
wasimamie na kutoa elimu kwa jumuiya zote na hiyo itasaidia miradi ya maji
inayotekelezwa na serikali kukaa kwa muda mrefu na kuwahudumia wananchi kama
ilivyokusudiwa.
Naye mkuu wa chuo cha maji Dr Shija Kazumba
amesema kuwa chuo chake kinakabiliwa na upungufu wa watumishi hali inayofanya
chuo hicho kushindwa kutimiza majukumu yake kama ipasavyo.
NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI MH. JUMAA AWESO AMEWATAKA WAHANDISI WA MAJI KATIKA HALMASHAURI ZOTE KUSIMAMIA VYEMA MIRADI YA MAJI.
Reviewed by safina radio
on
November 23, 2017
Rating:

No comments