IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA TETEMEKO NCHINI IRANI YAFIKA 350

TAREHE 14-11-2017

Idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko la ardhi katika mpaka wa Iran na Iraq, imefikia 350.

Wizara ya mambo ya ndani ya Iran imesema watu wengine elfu sita na mia sita  wamejeruhiwa na tetemeko hilo lililotokea jana jioni na lililokuwa na ukubwa wa 7.3 katika kipimo cha Richta,huku  majimbo ya Iran ya Kermansha na Illam ndiyo yameathiriwa vibaya na tetemeko hilo la ardhi.

Msemaji wa shirika la kukabiliana na majanga nchini Iran, Behnam Saeedi amesema waliojeruhiwa wamepelekwa kwenye vituo vya matibabu.


 Kituo cha Marekani kinachohusika na utafiti wa kijiolojia, kimesema eneo kuu la tetemeko hilo lilikuwa kwenye mkoa ulioko milimani nchini Iraq, umbali wa kilomita mia mbili  kaskazini mashariki mwa Baghdad na kilomita mia nne magharibi mwa Tehran.
IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA TETEMEKO NCHINI IRANI YAFIKA 350 IDADI YA WALIOFARIKI KATIKA TETEMEKO NCHINI IRANI YAFIKA 350 Reviewed by safina radio on November 14, 2017 Rating: 5

No comments