KONGAMANO LA KITAIFA LA VIJANA KATIKA UKUMBI WA REDIO SAFINA MBAUDA JIJINI ARUSHA.
Mpendwa mwana wa Mungu asante kwa kuwa sehemu ya mwanafamilia ya Safina Ministry and Fellowship.
Tunaomba radhi mpendwa mwanafamilia wetu kwa kuweza kupata tangazo hili kimakosa hapo awali, na kwa sasa tunapenda kuku arifu kuwa tarehe ya hapo awali, 23 Desemba, mwaka huu naakuwa tarehe 09 Desemba 2017.
Hivyo basi, kijana wa Kitanzania na mwanafamilia wa safina ni majira na nyakati sasa kuweza kupata fursa ya kupakwa mafuta kwa pembe ili kuinua huduma, karama na ndoto iliyo ndani yako.

Maana Mungu anahitaji moyo uliomuelekea yeye katika Roho na kweli ili aweze kutia baraka yake ndani yako kwa lengo la kutukuzwa, kusifiwa na kupewa utukufu kwa matendo yako, mafanikio na fahari yako.
Huduma ya Redio Safina imekuandalia kongamano la kitaifa la Vijana katika ukumbi wake uliopo Mbauda Jijini Arusha.
Sasa wewe Kijana wa Kiume na wa Kike, MTanzania popote ulipo unakaribishwa kushiriki katika Kongamano hili la kipekee kwa ajili yako ili Mungu akakuoneshee utukufu wake kama alivyonyesha ukuu wake katika familia ya Yese kwa kumteua Daudi kuwa Mfalme.
Hata hivyo, kijana Mtanzania Mungu bado anakusikia unapo mlilia na kumuita. Mwanzo 21:17-19 inatueleza kuwa
Mungu akasikia sauti ya kijana. ...... Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. Ondoka, ukamwinue...... Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
ZINGATIA, kila kijana katika Kongamano hilo anatakiwa kuwa na mshumaa kama ishara ya kuonyesha kutozima kwa maono yako wakati ukiwa umewashwa na maji ambapo wanaweza kuyapata ukumbi wa Safina Radio. Maji ni ishara ya kichocheo cha maono waliyonayo vijana.
Hivyo, usipange kukosa.
KONGAMANO LA KITAIFA LA VIJANA KATIKA UKUMBI WA REDIO SAFINA MBAUDA JIJINI ARUSHA.
Reviewed by safina radio
on
November 11, 2017
Rating:

No comments