MKUU WA MKOA WA PWANI EVARIST NDIKILO AWAAGIZA WAKUU WOTE WA WILAYA MKOANI HUMO KUPIGA MARUFUKU UTOROSHWAJI WA KOROSHO.
TAREHE 1-11-2017
Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mhandisi Evarist Ndikilo amewaagiza Wakuu wa Wilaya zote mkoani humo kupiga marufuku utoroshwaji wa zao la
Korosho unaofanywa na baadhi ya wafanyabiashara ambao wanahujumu
uuzwaji wa zao hilo kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani.
Mhandisi Ndikilo ametoa
agizo hilo wilayani Mkuranga mkoani humo wakati wa kikao cha Bodi ya Korosho na
kuongeza kuwa hatua ya wafanyabiashara hao kuhujumu mfumo huo inamkandamiza
mkulima.
Hata hivyo baadhi ya
Wajumbe wa Bodi ya Korosho Mkoani Pwani mbali na kupongeza juhudi za serikali
za kuboresha upatikanaji wa pembejeo na dawa ya Salfa pia wamelalamikia
upatikanaji wa magunia yanayofaa kuhifadhia zao hilo.
MKUU WA MKOA WA PWANI EVARIST NDIKILO AWAAGIZA WAKUU WOTE WA WILAYA MKOANI HUMO KUPIGA MARUFUKU UTOROSHWAJI WA KOROSHO.
Reviewed by safina radio
on
November 01, 2017
Rating:

No comments