RAIS WA NIGERIA AWAFUKUZA KAZI MAAFISA WAWILI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

TAREHE 31-10-2017

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amewafukuza kazi maafisa wawili wa ngazi ya juu wa serikali kwa tuhuma za kuhusika na rushwa, miezi sita baada ya kuwasimamisha kazi.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Nigeria, Balozi Ayo Oke amefukuzwa kazi kwa tuhuma za kujipatia fedha taslimu zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 43.

Naye afisa wa ngazi ya juu wa umma na katibu wa baraza la mawaziri, Babachir Lawal, amefukuzwa kazi baada ya kutuhumiwa kubadilisha matumizi ya fedha za miradi ya misaada zilizopangwa kutumika kwenye maeneo ambayo yameharibiwa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram.


Rais Buhari aliyechaguliwa mwaka 2015, aliahidi kupambana na rushwa, lakini vyama vya upinzani vinamshutumu kwa kuwalenga zaidi wapinzani wake kisiasa.
RAIS WA NIGERIA AWAFUKUZA KAZI MAAFISA WAWILI KWA TUHUMA ZA RUSHWA RAIS  WA  NIGERIA AWAFUKUZA KAZI MAAFISA WAWILI KWA TUHUMA ZA RUSHWA Reviewed by safina radio on October 31, 2017 Rating: 5

No comments