MKUU WA MKOA WA ARUSHA BW. MRISHO GAMBO AMEWAOMBA WADAU MBALIMBALI KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI.
TAREHE 24-10-2017
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo amewaomba wadau
mbalimbali kuendelea kuunga mkono jitihada za Mh. Raisi wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kwa kutoa vifaa vya ujenzi ili kuweza kukamilisha ujenzi wa nyumba
za askari zilizoungua hivi karibuni.
Bw Gambo ameyasema hayo leo alipotembelea ujenzi wa nyumba hizo
unaoendelea katika kata ya Sekei ambapo amewashukurù wadau waliojitolea mpaka
sasa na kuwaomba wengine kujitokeza katika kusaidia vifaa mbalimbali ili askari
hao waweze kuishi kwenye mazingira mazuri.
Aidha Gambo amemshukuru mwenyekiti wa kamati ya ujenzi kwa upande
wa wadau binafsi Bw. Hans Paul kwa kuacha shughuli zake na kujitoa kusimamia
ujenzi huo.
Pia amemshukuru raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Magufuli kwa kuanzisha mchakato wa ujenzi wa nyumba hizo ambapo tarehe 16
mwezi wa tisa baada ya nyumba hizo kuteketea kwa moto alitoa kiasi cha shilingi
milioni mia mbili sitini.
Hata hivyo kufikia sasa wadau mbalimbali wamejitokeza kutoa
misaada mbalimbali ikiwemo vyakula, saruji, mabati na fedha ambapo mpaka sasa
nyumba hizo zenye uwezo wa kuhîfadhi familia 33 zimefikia hatua ya
lenta.
MKUU WA MKOA WA ARUSHA BW. MRISHO GAMBO AMEWAOMBA WADAU MBALIMBALI KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI.
Reviewed by safina radio
on
October 24, 2017
Rating:

No comments