MAELFU WAANDAMANA HUKO BARCELONA KUPINGA CATALONIA KUJITENGA

TAREHE 09-10-2017


Mamia kwa maelfu ya watu wamemiminika katika mitaa ya mji mkuu wa Catalonia, Barcelona wameandamana wakipinga jimbo hilo kujitenga kutoka Uhispania na kuonyesha ni kwa namna gani mkoa huo umegawanyika kuhusu suala hilo.

Polisi wa ndani wamekadiria kwamba waandamanaji elfu thelathini na tano  waliokuwa wamebeba bendera ya Uhispania na Catalonia na mabango yaliyokuwa na ujumbe kwamba Catalonia ni Uhispania na pamoja tuna nguvu, wameshiriki maandamano hayo.


Maandamano hayo ya  mjini Barcelona yaliandaliwa na kundi linalopinga mkoa huo kujitenga la Catalan Civil society ili kuhamasisha kile wanachoamini ni idadi kubwa ya walio kimya wanaopinga suala la kujipatia uhuru.
MAELFU WAANDAMANA HUKO BARCELONA KUPINGA CATALONIA KUJITENGA MAELFU   WAANDAMANA  HUKO  BARCELONA  KUPINGA CATALONIA  KUJITENGA Reviewed by safina radio on October 09, 2017 Rating: 5

No comments