POLISI NCHINI MAREKANI KUFANYA UCHUNGUZI WA VIFO VYA WATU ZAIDI YA 59

TAREHE 03-10-2017



Polisi wanajaribu kugundua sababu ya ufyatuaji mkubwa wa risasi uliosababisha vifo vya watu 59 na kuwajehi wengine 527 kwenye warsha moja huko Las Vegas nchini Marekani.

Mtu mwenye silaha Stephen Paddock, mwenye umrii wa miaka 64, alifyatua risasi kutoka ghorofa ya 32 ya hoteli ya Mandalay Bay,wakati warsha moja ya mziki Jumapili ukiendelea usiku huko nchini Marekani.

Polisi walipata bunduki 23 kwenye chumba chake cha hoteli na zingine 19 na vilipuzi nyumbani kwake huko Nevada lakini hadi sasa hakuna sababu ya hatua yake hiyo iliyoibuka.

Wachunguzi hawajapata uhusiano wowote na ugaidi licha ya kundi la Islamic State kudai kuhusika.


Baadhi ya wachunguzi wamedai mtu huyo kuwa na matatizo ya kisaikolojia lakini hilo bado halijathibitishwa.
POLISI NCHINI MAREKANI KUFANYA UCHUNGUZI WA VIFO VYA WATU ZAIDI YA 59 POLISI  NCHINI  MAREKANI  KUFANYA  UCHUNGUZI  WA  VIFO  VYA WATU ZAIDI  YA  59 Reviewed by safina radio on October 03, 2017 Rating: 5

No comments