MUUNGANO WA UPINZANI NCHINI KENYA WAAHIRISHA MAANDAMANO NCHINI HUMO

TAREHE 7-10-2017

Muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) umefutilia mbali maandamano ambayo yalikuwa yamepangwa kufanyika leo nchini  humo kushinikiza mageuzi katika tume ya uchaguzi.
Muungano huo, kupitia taarifa, umesema umechukua hatua hiyo kupata fursa ya kuomboleza watu ambao wameuawa kwenye maandamano ya awali,ambapo maandamano hayo yataendelea tena siku ya Jumatano.

Nasa, muungano unaoongozwa na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, ulikuwa umeahidi kufanya maandamano kila siku kushinikiza mageuzi katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio.
MUUNGANO WA UPINZANI NCHINI KENYA WAAHIRISHA MAANDAMANO NCHINI HUMO MUUNGANO  WA  UPINZANI  NCHINI  KENYA  WAAHIRISHA MAANDAMANO NCHINI HUMO Reviewed by safina radio on October 17, 2017 Rating: 5

No comments