WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII DK. KIGWANGALA AMEITAKA MAMLAKA YA NGORONGORO KUKAA NA WAFUGAJI

TAREHE 27-10-2017


Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangala ameagiza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kukaa pamoja na Wafugaji wa Ngorongoro ili kuhakikisha wanamaliza migogoro na changamoto zote zinazowakabili wananchi wa eneo hilo.

Dk. Kigwangala ameyasema wakati akizungumza na Watendaji pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi katika Mamlaka hiyo,ambavyo  amesema kuwa ni vyema Wafanyakazi wakashirikiana ili kuhakikisha wana uhusiano wa karibu katika utendaji kazi badala ya Kulaumiana.


Kwa upande wke Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dk. Fredy Manongi amesema watahakikisha wanakutana na Baraza la Wafugaji la Ngorongoro na kujadili masuala muhimu ya kisera ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
WAZIRI WA MALI ASILI NA UTALII DK. KIGWANGALA AMEITAKA MAMLAKA YA NGORONGORO KUKAA NA WAFUGAJI WAZIRI  WA  MALI ASILI  NA UTALII DK. KIGWANGALA AMEITAKA   MAMLAKA  YA  NGORONGORO  KUKAA NA WAFUGAJI Reviewed by safina radio on October 27, 2017 Rating: 5

No comments