MAREKANI YAITAKA CUBA KUWAONDOA WAFANYAKAZI 15 KATIKA UBALOZI WAKE JIJINI WASHINGTON
TAREHE-10-2017
![]() |
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA MAREKANI REX TILLERSON |
Marekani imeitaka Cuba kuondoa wafanyakazi 15 wa
ubalozi wake mjini Washington kwa muda usiozidi siku saba, kufuatia madai kuwa
Cuba imekuwa ikifanya mfululizo wa mashambulizi ambayo yaliathiri afya za
wanadiplomasia 22 wa Marekani nchini Cuba mnamo miezi ya hivi karibuni.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson
amesema hatua hiyo ya Marekani imechukuliwa kutokana na kushindwa kwa Cuba kutilia
maanani utaratibu wa kuwalinda wanadiplomasia wa nchi yake.
Wakati huo huo, Marekani ilitangaza Ijumaa iliyopita
kuwa inaondoa theluthi mbili ya wafanyakazi wa ubalozi wake mjini Havana, na
imetoa tahadhari kwa wamarekani wanaotaka kusafiri kuelekea kisiwani Cuba.
MAREKANI YAITAKA CUBA KUWAONDOA WAFANYAKAZI 15 KATIKA UBALOZI WAKE JIJINI WASHINGTON
Reviewed by safina radio
on
October 04, 2017
Rating:

No comments