RAIS WA ZANZIBAR DR. ALL MOHAMED SHEIKN KUFUNGUA MKUTANO WA SIKU MBILI WA WADAU WA KILIMO JIJINI ARUSHA
TAREHE 04-10-2017
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr All Mohamed Sheikn anatarajiwa kufungua mkutano wa siku mbili wa kimataifa wa wadau wa kilimo cha mboga mboga,matunda na maua utakaofanyika jijini Arusha.
Hayo yamesemwa na meneja mkuu (maendeleo ) kutoka Asasi ya kilimo cha mboga mboga,matunda na maua (TAHA) ya jijini Arusha Bw Antony Chamanga wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na mkutano huo unaotarajiwa kuanza october 9 mwaka huu jijini Arusha.
Chamanga amesema kuwa katika mkutano huo ambao utakuwa wa kimataifa wadau wa sekta hiyo wataweza kujadili na kukubaliana maswala ya msingi ya kuendeleza sekta ya kilimo ikiwemo namna ya kuwafanya wakulima waweze kuzitambua teknolojia mpya za kisasa ambazo zitawawezesha waweze kuongeza uzalishaji katika kilimo chao.
Pia katika mkutano huo wadau hao wataangalia na kujadili ufikiaji wa masoko ya mazao hayo ya mboga mboga kwani masoko ni moja ya changamoto inayowakabili wakulima wa sekta hiyo hivyo wadau kutoka taasisi mbambali wataweza kutoa uzoefu kwa wakulima wauze wapi mazao yao na namna ya kuweza kufikia fursa za masoko zilizopo nje ya nchi na hata ndani ya nchi.
Hata hivyo zaidi ya wadau 200 wa sekta ya kilimo hapa nchini wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo.
![]() |
RAIS WA ZANZIBAR DR. ALL MOHAMED SHEIKN |

Reviewed by safina radio
on
October 04, 2017
Rating:

No comments