GEORGE WEAH AZIDI KUONGOZA KATIKA UCHAGUZI WA LIBERIA
13-10-2017
Tume ya uchaguzi nchini Liberia inasema mchezaji wa
zamani wa kimataifa wa kandanda George Weah anaongoza katika matokeo ya awali
ya wa rais nchini humo huku makamu wa rais Joseph Boakai naye pia akiongoza
katika mkoa anakotoka huku matokeo hayo yakionesha kura katika maeneo mengi
hazijahesabiwa.
Hata hivyo Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo
Jerome Korkoya ametahadharisha kuwa matokeo hayo ya awali ya urais yanayoonesha
mgombea wa chama cha Congress for Democtaric Change George Weah kuwa anaoongoza
ni ya sehemu ndogo tu kati ya vituo vyote vya kupigia kura nchini humo.
Wafuasi wa mgombea wa tatu kwenye kinyanganyiro hicho
wamekuwa wakidai kuwa kumekuwepo na kasoro katika uchaguzi huo huku vyama vya
siasa vikionesha wasiwasi juu ya kasoro ambazo zimechangia kuchelewa kutangazwa
kwa matokeo.
Hata hivyo Novemba 7 mwaka huu ndiyo siku iliyopangwa
kufanyika uchaguzi wa marudio iwapo hakuna mgombea atakayeshinda kwa kiwango
cha asilimia 50 cha kura za urais miongoni mwa wagombea 20 wanaowania nafasi
hiyo.
GEORGE WEAH AZIDI KUONGOZA KATIKA UCHAGUZI WA LIBERIA
Reviewed by safina radio
on
October 13, 2017
Rating:

No comments