CHUO KIKUU NCHINI KENYA CHAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA

TAREHE 04-10-2017



Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya kimefungwa kwa muda usiojulikana, kufuatia maandamano ya wanafunzi dhidi ya ukatili wa polisi.

Naibu mkuu wa chuo hicho Peter Mbithi amesema kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, kwamba kufungwa huko kumetokana na kuzidi kuzorota kwa hali ya usalama, akiongeza kuwa wanafunzi 26 walikuwa wamejeruhiwa na polisi walioingia chuoni, na kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waliokuwa wakiandamana.

Maandamano hayo  yalianza wiki iliyopita, baada ya kukamatwa kwa aliyewahi kuwa rais wa wanafunzi wa chuo kikuu hicho cha Nairobi Babu Owino, ambaye alikuwa ameshinda kinyang'anyiro cha ubunge, akimuunga mkono kiongozi wa upinzani Raila Odinga.


Hata hivyo Bw Odinga atapambana tena na Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mpya wa rais utakaofanyika Octoba 27 mwaka huu, baada ya matokeo ya uchaguzi wa kwanza kubatilishwa na mahakama kuu.
CHUO KIKUU NCHINI KENYA CHAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA CHUO KIKUU  NCHINI  KENYA  CHAFUNGWA   KWA MUDA  USIOJULIKANA Reviewed by safina radio on October 04, 2017 Rating: 5

No comments