MADRID YALAZIMISHWA SARE IKIWA NYUMBANI

TAREHE 18-10--2017
Tottenham ilifunga bao lake la kwanza dhidi ya Real Madrid baada ya kushindwa kufanya hivyo katika mechi nneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image caption
Tottenham Hotspur ilionyesha kwamba inaweza kucheza katika kiwango cha juu , alisema mshambuliaji Harry Kane baada ya timu yake kupiga hatua kubwa katika kombe la vilabu bingwa kwa kujipatia alama moja ugenini Real madrid.
Spurs iliwalazimu mabingwa hao mara 12 wa Ulaya kupigania sare ya 1-1 katika uwanja wa Bernabeu siku ya Jumanne.
Timu hiyo ya ligi ya Uingereza iliongoza pale Beki wa Madrid Raphael Varane alipolazimika kujifunga kufuatia krosi ya Serge Aurier.
Mabingwa hao wa Uhispania hatahivyo walisawazisha kabla ya kipindi cha kwanza wakati Aurier alipomchezea visivyo Toni Kroos katika eneo hatari na kusababisha penalti iliofungwa na Cristiano Ronaldo.

MADRID YALAZIMISHWA SARE IKIWA NYUMBANI MADRID YALAZIMISHWA SARE IKIWA NYUMBANI Reviewed by safina radio on October 18, 2017 Rating: 5

No comments