MUGURUZA ATUPWA NJE CHINA OPEN

TAREHE 03-10-2017


Garbine Muguruza
Image captionGarbine Muguruza

Mchezaji nambari moja kwa upande wa kina dada Garbine Muguruza amejiondoa katika michuano ya China Open.
Muguruza mwenye miaka 23 alipoteza seti ya kwanza kwa 5-1 mbele ya Barbora Strycova wa Jamhuri ya Czech.
Mshindi huyo wa michuano ya Wimbledon aliumia kiwiko cha mkono na kumfanya ashindwe kusonga mbele zaidi.
Baada ya timu ya madaktari kuwasili, ilisemekana kwamba hatoweza kumalizia ngwe iliyokuwa imesalia.
Muguruza amesema hakupenda kabisa kuishia katikati ya michuano hiyo.
MUGURUZA ATUPWA NJE CHINA OPEN MUGURUZA ATUPWA NJE CHINA OPEN Reviewed by safina radio on October 03, 2017 Rating: 5

No comments