BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA KUPIGA KURA LEO JUU YA MASHAMBULIZI YA KEMIKALI NCHINI SYRIA.

TAREHE 24-10-2017


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, linatarajiwa kupiga kura leo, juu ya kupanua uchunguzi wa nani alihusika na mashambulizi ya silaha za kemikali nchini Syria.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amethibitisha kuwa wajumbe wa baraza hilo watapigia kura, azimio la kurefusha muda wa kamati ya pamoja ya uchunguzi ilioidhinishwa na baraza hilo, pamoja na ujumbe wa kutafuta ukweli wa shirika la kuzuwia kuenea kwa silaha za kemikali OPCW, kwa mwaka mwingine mmoja.

Mwaka 2013, Baraza la Usalama lilipitisha azimio linaloitaka Syria kuharibu silaha zake za kemikali na kukomesha mashambulizi kama hayo.

Zaidi ya watu 80 waliuawa katika shambulizi la gesi ya sarin katika mji wa waasi mwezi Aprili, ambalo wachunguzi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, wanaoendesha uchunguzi tofauti, wanasema lilifanywa na jeshi la anga la Syria.
BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA KUPIGA KURA LEO JUU YA MASHAMBULIZI YA KEMIKALI NCHINI SYRIA. BARAZA LA USALAMA   LA  UMOJA  WA  MATAIFA  KUPIGA KURA  LEO JUU  YA  MASHAMBULIZI  YA   KEMIKALI   NCHINI  SYRIA. Reviewed by safina radio on October 24, 2017 Rating: 5

No comments