SERIKALI MKOANI MOROGORO KUWACHUKULIA HATUA WATUMISHI WATAKAOHUJUMU RUZUKU YA PEMBEJEO

TAREHE 19-10-2017


Serikali mkoani Morogoro imesema haitasita kuwachukulia hatua kali watumishi wote kuanzia ngazi ya kijiji hadi Mkoa watakaobainika kuhujumu ruzuku ya pembejeo za kilimo na kusababisha hasara kwa wakulima na serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Dk. Kebwe Stivin Kebwe ametoa onyo hilo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya chakula kwa mkoa huo kwa 2016-2017

Aidha, Dk. Kebwe amesema kuwa wamefanya mawasiliano na wizara ya kilimo kupata orodha ya watu waliofanya uhujumu katika pembejeo, ili kuwachukulia hatua huku akitoa agizo kwa wakurugenzi wote wa halmashauri za mkoa huo wachukue hatua kwa wasimamizi wote wa pembejeo waliofanya vitendo hivyo.


Vile vile, Dk. Kebwe ameongeza kuwa kutokana na kero ya soko la mbaazi serikali ya mkoa huo imeshampata mwekezaji  atakaye jenga kiwanda kikubwa cha kusaga zao hilo huku akiwaonya wananchi kutokutumia mazao kwa matumizi yasiofaa ikiwemo kwenye ngoma na pombe.
SERIKALI MKOANI MOROGORO KUWACHUKULIA HATUA WATUMISHI WATAKAOHUJUMU RUZUKU YA PEMBEJEO SERIKALI   MKOANI  MOROGORO   KUWACHUKULIA  HATUA  WATUMISHI  WATAKAOHUJUMU  RUZUKU YA  PEMBEJEO Reviewed by safina radio on October 19, 2017 Rating: 5

No comments