MAREKANI YAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA NA KOREA KUSINI

TAREHE 11-10-2017
Marekani kwa mara nyingine imefanya mazoezi ya kijeshi kwa pamoja na Korea Kusini, ambapo ndege zake mbili za kivita za kuangusha mabomu zimepaa juu ya rasi ya Korea.
Ndege hizo za kutekeleza mashambulizi aina ya B-1B zimepaa angani pamoja na ndege za kivita za Korea Kusini aina ya F-15K.
Ndege hizo zimefanya  mazoezi ya kurusha makombora kutoka angani hadi ardhini katika maji ya bahari ya Korea Kusini.
Mazoezi hayo yamefanyika huku wasiwasi na uhasama kati ya Marekani na Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa nyuklia ukizidi.
Pyongyang  ilitekeleza jaribio lake la sita la silaha za nyuklia na pia imerusha makombora kupitia anga ya Japan mara mbili miezi ya karibuni.
Jeshi la Korea Kusini limesema Ndege hizo za Marekani zilipaa kutoka kisiwa chake cha Guam katika Bahari ya Pacific Jumanne usiku, kabla ya kuingia anga ya Korea Kaskazini na kufanya mazoezi katika Bahari ya Mashariki na Bahari ya Manjano.

Hata hivyo ikulu ya White House imesema  Rais wa Marekani Donald Trump alikutana na maafisa wakuu wa usalama Jumanne usiku kujadili njia za kukabili vitisho vya Korea Kaskazini.
MAREKANI YAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA NA KOREA KUSINI MAREKANI YAFANYA MAZOEZI YA PAMOJA NA KOREA KUSINI Reviewed by safina radio on October 11, 2017 Rating: 5

No comments