MADEREVA MKOANI ARUSHA WATAKIWA KUTII SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

TAREHE 02-10-2017



Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha Bw Nuru Seleman amewataka madereva kuheshimu na kutii sheria za usalama wa barabarani  ili kuepukana na ajali zinazoweza kuzuilika.

Bw Selemani ametoa kauli hiyo jijini Arusha wakati akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi waliojitokeza katika maadhimisho ya siku ya SUMATRA iliyoandaliwa na baraza la ushauri la mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu Tanzania.

Amesema kuwa jeshi la polisi halitawavumilia madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani,na moja ya hatua watakazochukuliwa kuwa ni pamoja na kufutiwa leseni zao,ambapo pia amelishukuru baraza la ushauri la mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu SUMATRA kwa kuanzisha vilabu vya wanafunzi vinavyosaidia kuelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi bora ya vyombo vya usafiri


Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza hilo mkoa wa Arusha ameishukuru serikali kwa ushirikiano wanaoutoa kwa baraza hilo,ambapo pia ametumia maadhimisho hayo kumuomba mkuu huyo wa usalama barabarani kusaidia kusimamia zoezi la utoaji tiketi ili abiria aweze kupata haki yake pale tatizo litakapotokea.
MADEREVA MKOANI ARUSHA WATAKIWA KUTII SHERIA ZA USALAMA BARABARANI MADEREVA   MKOANI   ARUSHA   WATAKIWA    KUTII   SHERIA  ZA   USALAMA   BARABARANI Reviewed by safina radio on October 02, 2017 Rating: 5

No comments