SERIKALI YATENGA FEDHA ILI KUWAPATIA VIJANA UJUZI KUHUSU UWEKEZAJI
TAREHE 19-10-2017
![]() |
MH.JENISTA MUHAGAMA |
Waziri wa
Kazi Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mh. Jenista Muhagama amesema
serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuwapatia ujuzi vijana kuhusu uwekezaji wa
viwanda ili kufikia uchumi wa kati.
Mh.
Muhagama ameyasema hayo jijini Arusha wakati akifungua mkutano wa 7 wa Wadau wa
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF.
Aidha,
Mh. Muhagama amesema kuwa lengo la kuwapatia ujuzi vijana hao linatokana na
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuwekeza katika viwanda 27 na kutoa ajira laki tatu.
Waziri
Muhagama amewahakikishia wadau hao kuwa serikali imejipanga kulipa madeni yote
ambayo inadaiwa na amewataka waajiri walipe michango, madeni, na
malimbikizo yao.
Naye,
Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya NSSF Prof. Samwel Wangwe amesema wameanzisha
utaratibu kuwapokea askari wa Jeshi la Ulinzi wa Tanzania ili wanufaike kupata
matibabu yao na familia zao.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa wizara ya Kazi, Ajira Na Vijana Anthon Mavunde
amesema kuwa suala la wanachama kujitoa katika Mifuko ya hifadhi ya Jamii ni
changamoto inayoikabili Mifuko hiyo.
SERIKALI YATENGA FEDHA ILI KUWAPATIA VIJANA UJUZI KUHUSU UWEKEZAJI
Reviewed by safina radio
on
October 19, 2017
Rating:

No comments