WAKENYA WANAPIGA KURA LEO KUMCHAGUA RAIS
TAREHE 26-10-2017
Wananchi wa kenya leo wanashiriki katika zoezi la kupiga kura ya urais
katika uchaguzi mpya baada ya mahakama ya juu ya nchini humo kuubatilisha
ushindi wa rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi wa mwezi Agosti mwaka huu.
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amewahimiza
wafuasi wake kutoshiriki katika uchaguzi huo wa leo na hali ya wasiwasi
imetanda huku ikihofiwa kwamba huenda kukazuka vurugu.
Wafuasi wa rais Uhuru Kenyatta, ambaye anawania awamu ya pili ya uongozi wa
taifa la Kenya hapo jana walisherehekea pale walipopata habari kwamba zoezi la
kupiga kura litaendelea baada ya Mahakama ya juu kushindwa kuendelea kusikiliza
na kutoa maamuzi ya kusitisha kura hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta amesema hali ya
usalama itaimarishwa nchini kote na amewataka Wakenya kwenda kupiga kura huku
wakizingatia haki za wale ambao hawataki kushiriki katika upigaji kura.
WAKENYA WANAPIGA KURA LEO KUMCHAGUA RAIS
Reviewed by safina radio
on
October 26, 2017
Rating:

No comments