UELEWA MDOGO KUHUSU MASUALA YA LISHE WASABABISHA KUWEPO UTAPIA MLO.
TAREHE 16-10-2017
Imeelezwa
kuwa uelewa mdogo wa masuala ya lishe miongoni mwa wananchi na viongozi umeendelea
kuwa changamoto katika kukabilina na utapia mlo kwa watoto walio na umri chini
ya miaka mitano nchini.
Hayo
yameelezwa na mtaalamu wa Lishe kutoka ofisi ya rais TAMISEMI Bw Muta Waibe katika uzinduzi wa mpango wa
uongezaji wa virutubishi kwenye unga ambao unalenga kupunguza matatizo ya
utapiamlo pamoja na udumavu kwa watoto na akinamama wote wenye umri wa kujifungua
uliofanyika huko mkoani Iringa.
Aidha,
Bw. Waibe ameeleza kuwa kutokana na serikali pamoja na wadau kutowekeza katika
elimu ya lishe kumesababisha kuwa na kizazi kisichokuwa na uelewa wa mambo
hivyo mikakati ya maendeleo yaliyopangwa kwa muda mrefu kukwama kutokana na
kufanya mambo kinyume.
Kwa
upande wake mkurugenzi Msaidizi wa mradi wa kuongeza virutubisho wa nafaka
James Lock amesema mradi huo unatoa ruzuku kwa wasindikaji wa kati wenye uwezo
wa kuzalisha hadi tani kumi kwa siku.
Hata
hivyo virutubishi vinnavyoongezwa ni pamoja vile vya madini ya chuma, madini ya
joto, protini, na vitamin B, ambavyo kukosekana kwake kunasababisha udumavu,
utapia mlo, mgongo wazi pamoja na vichwa vikubwa.
UELEWA MDOGO KUHUSU MASUALA YA LISHE WASABABISHA KUWEPO UTAPIA MLO.
Reviewed by safina radio
on
October 16, 2017
Rating:

No comments