TAREHE 25-10-2017 Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage caption
Claudio Bravo aliwafaa sana Manchester City baada ya kuwasaidia kuilaza Wolves kupitia mikwaju ya penalti katika Kombe la Carabao na kuwasaidia kufika robofainali.
Bravo, alifanya kazi ya ziada kuzuia wasifungwe bao muda wa kawaida wa mechi, na aliendeleza hilo kwa kuzuia mikwaju ya Alfred N'Diaye na Conor Coady wakati wa matuta ya baada ya mechi baada ya mchezo huo kumalizika kwa sare tasa.
City walifunga mikwaju yao yote, mkwaju wa Sergio Aguero ukiwa wa ushindi.
Wolves walikuwa ndiyo timu ya kwanza kuwalemea viongozi hao wa Ligi ya Premia na kuwazuia kufunga msimu huu.
Wolves, wamo alama mbili mbele kileleni katika Ligi ya Championship na walicheza vizuri sana mechi hiyo iliyochezewa Etihad, wakishangiliwa na mashabiki wao wapatao 6,000.
Kabla ya kufika Etihad, vijana hao wa Nuno Espirito Santo walikuwa wamefungwa mabao 13 pekee katika michezo 16 msimu wote.
City watakuwa ugenini dhidi ya West Bromwich Albion Jumamosi wakilenga kuendeleza ubabe wao Ligi ya Premia.
Wolves nao watakuwa ugenini kucheza dhidi ya QPR uwanjani Loftus Road katika ligi ya Championship siku hiyo.
MANCHESTER CITY YASONGA MBELE KATIKA KOMBE LA KARABAO
Reviewed by safina radio
on
October 25, 2017
Rating: 5
No comments