SERIKALI IMELIPA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MIA MOJA NA TISINI IKIWA NI MADENI YA WAKANDARASI NA WAZABUNI.

TAREHE  18-10-2017

NAIBU  WAZIRI  WA  FEDHA DK. ASHANTU  KIJAJU

Naibu Waziri wa Fedha na  Mipango Dk. Ashantu Kijaji amesema kuwa Serikali imekwisha lipa madeni ya wazabuni, wakandarasi na malimbikizo ya wafanyakazi yanayofikia kiasi cha Shillingi bilioni mia moja  na tisini katika kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi septemba mwaka huu baada ya kufanya uhakiki wa madeni mbalimbali inayodaiwa.

Dk. Kijaji ameyasema hayo mjini Bukoba wakati akizungumza na Jumuiya ya Wafanyakazi wa mkoa wa Kagera katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utendaji kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.

Waziri Kijaji amesema kuwa Wazabuni wameshalipwa kiasi cha shilingi bilioni 67.2, Wakandarasi wamelipwa kiasi cha shilingi bilioni 24.2 na watoa huduma mbalimbali wameshalipwa shilingi bilioni 38 na Watumishi wa umma bilioni 37 na Wadaiwa wakilipwa bilioni 24.

Aidha, Dk. Kijaji amesema kuwa hiyo ni dhamira njema iliyochukuliwa na serikali baada ya kumaliza zoezi la uhakiki kwa kudhibiti malipo ya madeni hewa yasiostahili kwa lengo la kufanikisha malipo hayo kwa wakandarasi waliotoa huduma kwa serikali


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa huo Bw. Seif Mkude ameipongeza serikali kwa jitihada za kuhamasisha ulipaji kodi kwa manufaa ya taifa kwa kuwa bila mapato nchi  haitaweza kuendelea.
SERIKALI IMELIPA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI MIA MOJA NA TISINI IKIWA NI MADENI YA WAKANDARASI NA WAZABUNI. SERIKALI   IMELIPA  ZAIDI  YA  SHILINGI  BILIONI MIA   MOJA   NA  TISINI  IKIWA  NI  MADENI   YA  WAKANDARASI   NA  WAZABUNI. Reviewed by safina radio on October 18, 2017 Rating: 5

No comments