RAIS WA TANZANIA MH. JOHN MAGUFULI KUFUNGUA MKUTANO WA 33 WA JUMUIYA ZA SERIKALI ZA MITAA KESHO

TAREHE 02-10-201

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. JOHN MAGUFULI

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Magufuli kesho anatarajiwa kufungua mkutano wa 33 wa jumuiya za serikali za mitaa (ALAT)Jijini Dar-es-salaam.

Hayo yameelezwa na meya wa jiji la Dar-es-salaam Mh Isaya Mwita wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini humo,ambapo amesema kuwa mkutano huo utawajumuisha wajumbe mbalimbali kutoka mikoa yote ya Tanzania.

Amesema kuwa mkutano huo utafungwa octoba 16 mwaka huu,ambapo pia wanatarajia kuwasilisha maombi rasmi kwa rais Magufuli ya kurejesha vyanzo vya mapato vilivyochukuliwa na serikali kuu viweze kurudishwa katika halmashauri ili ziweze kuongeza uwezo wa kujiendesha.


Kwa upande wake mmoja wa wajumbe wanaotarajia kuhudhuria mkutano huo Mh Haji Mnasi ambaye ni mkurugenzi wa wilaya ya Songwe amesema ku katika mkutano huo wanatarajia kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo namna ya kukabiliana na changamoto  wanazokabiliana nazo katika maeneo yao ya kazi pamoja na kubadilishana uzoefu.
RAIS WA TANZANIA MH. JOHN MAGUFULI KUFUNGUA MKUTANO WA 33 WA JUMUIYA ZA SERIKALI ZA MITAA KESHO RAIS  WA  TANZANIA  MH. JOHN  MAGUFULI KUFUNGUA  MKUTANO WA 33 WA JUMUIYA  ZA SERIKALI ZA MITAA KESHO Reviewed by safina radio on October 02, 2017 Rating: 5

No comments