WATU MIA MBILI SABINI NA SITA WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI NCHINI SOMALIA
TAREHE 16-10-2017
Viongozi mbalimbali duniani wameungana kulaani mashambulizi ya bomu nchini Somalia, ambayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya mia mbili sabini na sita, katika mji mkuu Mogadishu.
Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo
ya nje ya Marekani inasema kuwa nchi hiyo inalaani vikali mashambulizi hayo,
ikiahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Somalia kupambana na magaidi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza,
Boris Johnson, amesema nchi yake inalaani mashambulizi hayo ya woga, ambayo
yamegharimu maisha ya watu wengi.
Kauli kama hizo zimetolewa pia na Rais
Emmanuel Macron wa Ufaransa, Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, Rais Tayyip
Erdogan wa Uturuki, na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat,
pamoja na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.
Waziri wa Habari wa Somalia,
Abdilrahman Osman, amesema kuwa idadi ya waliopoteza maisha kwenye mashambulizi
hayo ya Jumamosi yanayohusishwa na kundi la kigaidi la al-Shabaab, imefikia mia
mbili sabini na sita huku wengine mia
tatu wakijeruhiwa.
WATU MIA MBILI SABINI NA SITA WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI NCHINI SOMALIA
Reviewed by safina radio
on
October 16, 2017
Rating:

No comments