WATU WAWILI WAUAWA NCHINI UFARANSA KWA KUDUNGWA VISU
TAREHE 02-10-2017
Kundi
linalojiita Dola la Kiislamu IS limedai kufanya shambulizi la kudunga visu
lililouwa watu wawili katika mji wa Kusini mwa Ufaransa wa Marseille, na
kuwajeruhi wengine kadhaa.
Polisi
wa kupambana na ugaidi wamesema wameanzisha uchunguzi kuhusu mashambulizi hayo,
wakiyatazama kama mauaji yenye uhusiano na ugaidi, na jaribio la kuuwa maafisa
wa serikali.
Kwa
upande wake rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron Kupitia ukurasa wake wa mtandao
wa Twitter, amesema ameghadhibishwa na mashambulizi hayo.
WATU WAWILI WAUAWA NCHINI UFARANSA KWA KUDUNGWA VISU
Reviewed by safina radio
on
October 02, 2017
Rating:

No comments