HALMASHAURI ZINAZODAIWA NA BODI YA MIKOPO ZATAKIWA KUREJESHA FEDHA HIZO

13-10-2017


Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI Seleman Jaffo amemwagiza Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa Nchini kuhakikisha kuwa Halmashauri zinazodaiwa na Bodi hiyo kwa muda mrefu zinarejesha fedha hizo ifikapo Desemba 30 mwaka huu.

Waziri Jaffo ametoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa Halmashauri kumi na mbili nchini hazijarejesha mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni mbili jambo ambalo limesababisha halmashauri nyingine kushindwa kukopeshwa.
Aidha, Waziri Jaffo amesema kuwa yeye amepewa dhamana ya kuiongoza ofisi hiyo, hivyo hangependa  wala kuridhika kwa utendaji wa chombo hicho ambacho kipo chini ya wizara yake kulegalega.

Mbali na hayo, Waziri Jaffo akamwagiza Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mikopo hiyo ya serikali za mitaa kwamba afuatilie wadaiwa wote sugu ambao wameshindwa kurejesha mikopo yao kama ilivyoainishwa katika mikataba sahihi na iliyohalali ya urejeshaji wa mikopo  hiyo.


Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Richard Mfugale amesema kuwa hadi kufikia Septemba 30 mwaka huu Bodi hiyo imekwisha toa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 9.7 za Kitanzania kwa Halmashauri hamsini na nne hapa nchini.
HALMASHAURI ZINAZODAIWA NA BODI YA MIKOPO ZATAKIWA KUREJESHA FEDHA HIZO HALMASHAURI  ZINAZODAIWA NA BODI YA MIKOPO ZATAKIWA KUREJESHA  FEDHA HIZO Reviewed by safina radio on October 13, 2017 Rating: 5

No comments