WATU ZAIDI YA 20 WAMEFARIKI KUTOKANA NA KIMBUNGA.

TAREHE 06-10-2017

Kimbunga kijulikanacho kama  Nate kimewaua watu zaidi ya 20 nchini Costa Rica, Nicaragua na Honduras huku kikielekea kaskazini upande wa Marekani.

Hali ya dharura imetangazwa katika mataifa kadha ya Amerika ya Kati ambapo watu zaidi ya 20 bado hawajulikani walipo,ambapo Kimbunga hicho kimesababisha mvua kubwa, maporomoko ya ardhi na mafuriko.

Barabara nyingi hazipitiki, madaraja yameporomoka na pia kimesababisha uharibifu mkubwa kwenye nyumba za watu na majengo.

Nchini Costa Rica, watu karibu laki nne hawana maji na maelfu wengine wameachwa bila makao na wanalala kwenye vyumba vya muda na watu zaidi ya sita wamethibitishwa kufariki katika taifa hilo.


Hata hivyo Watu watatu wameuawa nchini Honduras na kuna watu kadha ambao hawajulikani waliko.
WATU ZAIDI YA 20 WAMEFARIKI KUTOKANA NA KIMBUNGA. WATU   ZAIDI  YA  20  WAMEFARIKI   KUTOKANA  NA KIMBUNGA. Reviewed by safina radio on October 06, 2017 Rating: 5

No comments