RAIA WA LIBERIA WAPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS LEO
TAREHE 10-10-2017
Raia
wa Liberia leo wanapiga kura kumchagua kiongozi mpya atakayemrithi Rais Ellen
Johnson Sirleaf ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 12.
Wapiga
kura wana matumaini kuwa kiongozi mpya ataweza kuufufua uchumi wa taifa hilo,
na kudumisha amani baada ya nchi hiyo kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa
wenyewe kuanzia mwaka 1989 hadi 2003.
Wagombea
20 wanawania urais na miongoni mwao yupo mwanasoka maarufu wa zamani George
Weah, makamu wa rais wa sasa Jospeh Boakai, kiongozi wa muda mrefu wa upinzani
Charles Brumskine na mfanyabishara tajiri Alexander Cummings.
Mwanamke pekee anayewania urais ni MacDella
Cooper, ambaye ana ndoto za kufuata nyayo za Sirleaf ambaye ni mwanamke wa
kwanza kuwa rais Afrika,ambapo vituo vya kupigia kura vimefunguliwa
saa mbili asubuhi na vitafungwa saa kumi na mbili jioni, huku matokeo ya awali
yakitarajiwa kutangazwa saa 48 baada ya uchaguzi.
RAIA WA LIBERIA WAPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS LEO
Reviewed by safina radio
on
October 10, 2017
Rating:

No comments