WITO UMETOLEWA KWA WANANCHI HAPA NCHINI KUZINGATIA UPIMAJI WA ARDHI
TAREHE 01-10-2017
![]() |
NAIBU WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI MH. ANGELINA MABULA |
Serikali kupitia wizara ya ardhi
nyumba na maendeleo ya makazi imetoa
wito kwa wananchi wote hapa nchini
kuzingatia upimaji wa ardhi ili kusaidia kupatikana kwa makazi bora na
yaliyopangwa.
Wito huo umetolewa leo na naibu waziri wa Ardhi nyumba maendeleo
na makazi Mh Agelina Mabula wakati
akizungumza katika maadhimisho ya siku
ya Makazi Duniani yaliyofanyika jijini Dar-es-salaam.
Amesema kuwa endapo wananchi
watazingatia sheria ya makazi ya watu
pamoja na ya ardhi kutawaepusha
adha ya kusumbuliwa na kubomolewa nyumba
zao pale watakapobainika kuwa wamejenga maeneo yasiyoruhusiwa na serikali.
Ameongeza kuwa serikali kwa hivi
sasa imejipanga kuhakikisha kila
mwananchi anakuwa kwenye makazi yaliyo bora na hii itaepusha adha ya ujenzi usiofuata sheria kwa baadhi ya mikoa hapa nchini kwa kuwa wapo baadhi ya wananchi ambao wamekosa elimu namna ya kuwa na mipangilio mizuri ya iliyo makazi
yao
WITO UMETOLEWA KWA WANANCHI HAPA NCHINI KUZINGATIA UPIMAJI WA ARDHI
Reviewed by safina radio
on
October 02, 2017
Rating:

No comments