HUDUMA YA KESHO JUMANNE KATIKA UKUMBI WA RADIO SAFINA

TAREHE 02-10-2017

Imeelezwa kukaa mbele za Mungu kwa muda mrefu kunamfanya mtu aendelee kujiimarisha zaidi katika kila eneo ikiwa ni pamoja na kuidhibiti milango ya adui.

Huduma ya Redio Safina mkoani Arusha imekuandalia maombi maaliumu yakujifunza umuhimu wa kukaa mbele za Mungu kwa muda mrefu maombi ambayo yatafanyika katika ukumbi uliopo Mbauda kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita na nusu mchana.

Aidha, kwa kadiri unavyo kaa mbele za Mungu kwa muda Mrefu ndivyo unavyo tengeneza mahusiano mazuri baina yako wewe na Mungu.

Jumanne hii pia tutamshughulikia yule adui azuiaye baraka zako katika maeneo mbalimbali kama vile biashara ,elimu, kilimo, ufugaji, afya na hata ndoa sambamba na familia kwa ujumla.


Hata hivyo, unaalikwa wewe na jirani yako jumanne hii ili kukutana na muujiza wako ambapo watumishi wamejipanga kikamilifu kuhakikisha kila atakaye hudhuria katika maombi hayo anafunguliwa kila kifungo kinacho mkabili.
HUDUMA YA KESHO JUMANNE KATIKA UKUMBI WA RADIO SAFINA HUDUMA  YA KESHO  JUMANNE KATIKA  UKUMBI  WA  RADIO   SAFINA Reviewed by safina radio on October 02, 2017 Rating: 5

No comments