MANISPAA YA DODOMA YAFANIKIWA KUJENGA DAMPO LA KISASA LA TAKA

TAREHE 17-10-2017

Manispaa ya Dodoma imefanikiwa kujenga dampo la kisasa la taka ambalo lina uwezo wa kupokea tani 310 za taka huku  likiwa na uwezo wa kuzalisha ajira kwa wakazi wa manspaa hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika dampo hilo la Chidaya mhandisi msimamizi wa dampo hilo bwana Barnabas Faida amesema kuwa dampo hilo  linaendeshwa kwa kutumia mitambo hali inayosaidia kuweka  mji wa  Dodoma katika hali ya usafi.

Amesema kuwa ujenzi wa dampo hilo la kisasa umetumia kiasi cha zaidi ya bilioni mbili ambapo ujenzi wake ulianza mwaka 2011/2012 na kumalizika 2014 ambapo baada ya kumalizika lilianza rasmi kutumika mwaka 2016 ambapo uendeshaji wake unatumia mitambo minne na hivyo kuwezesha kukabiliana na taka zote zinazoingia katika dampo hilo.

Ameongeza kuwa kupitia dampo hilo limewezesha pia uzalishaji wa ajira kwa wakazi wa Dodoma kwani kwa mwezi wanalazimika kutumia kiasi cha shilingi milioni 20 kwa ajili ya kulipa vibarua  na hivyo kuwezesha wakazi hao kuweza kukabiliana na hali ngumu ya maisha..

Akizungumza kuhusiana na dampo hilo wasafirishaji wa taka akiwemo Bw Godgery Chorobi   amesema kuwa pamoja na kuwa dampo hilo lina faida kwa kutoa ajira ingawa  bado wanakabliwa na changamoto ya ubovu wa barabara ya upelekaji taka katika dampo hilo kutokana na miundombinu kuwa mibovu.
MANISPAA YA DODOMA YAFANIKIWA KUJENGA DAMPO LA KISASA LA TAKA MANISPAA   YA  DODOMA  YAFANIKIWA  KUJENGA  DAMPO  LA  KISASA LA TAKA Reviewed by safina radio on October 17, 2017 Rating: 5

No comments