ARGENTINA HATARINI KUKOSA KOMBE LA DUNIA NCHINI URUSI
06-10-2017
Argentina, na
mshambuliaji wao nyota Lionel Messi, wamo hatarini ya kukosa kufuzu kwa Kombe
la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1970 baada ya kutoka sare tasa na Peru.
Ni nchi nne pekee za
Amerika Kusini ambazo zinahakikishiwa nafasi katika michuano hiyo
itakayofanyika Urusi mwaka 2018.
Argentina wamo katika
nafasi ya sita wakiwa wamesalia na mechi moja pekee.
Mabingwa hao wa dunia
mara mbili ni lazima washinde mechi yao ya mwisho ya kufuzu dhidi ya Ecuador
kuwawezesha kufika angalau nafasi ya tano ambayo itawapatia fursa ya kucheza
mechi mbili za muondoano za kufuzu dhidi ya New Zealand.
Mkufunzi wa Argentina
Jorge Sampaoli amekiri kwamba mambo si mazuri lakini akaongeza kwamba ana imani
kuwa iwapo timu hiyo itacheza ilivyocheza dhidi ya Peru, basi watafuzu kwa
Kombe la Dunia.
Hata hivyo kocha Sampaoli
amesifu bidii ya mchezaji wa Barcelona
ambaye aliunda nafasi nyingi sana za kufunga ingawa wenzake walishindwa
kufunga.
Argentina, ambao
walimaliza wa pili Kombe la Dunia 2014, wanalingana kwa alama na Peru walio nafasi ya tano, alama
25.
Peru hata hivyo wako
mbele kwa sababu wamefunga mabao mengi.
ARGENTINA HATARINI KUKOSA KOMBE LA DUNIA NCHINI URUSI
Reviewed by safina radio
on
October 06, 2017
Rating:

No comments