WAFUASI WA UPINZANI NCHINI KENYA WAENDELEA KUANDAMANA
TAREHE 02-10-2017
Wafuasi wa muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance
(Nasa) wamejitokeza katika baadhi ya miji nchini humo kushinikiza kuondolewa
kazini kwa baadhi ya maafisa wakuu wa tume ya taifa ya uchaguzi.
Maafisa wa usalama
Kenya wamekuwa wakishika doria karibu na jumba la Anniversary Towers zilipo ofisi
za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) jijini Nairobi.
Muungano wa Nasa
ukiongozwa na Raila Odinga umetangaza maandamano ya kila Jumatatu na Ijumaa
kushinikiza kuondolewa kwa afisa mkuu mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba na maafisa
wengine wakuu kwa tuhuma kwamba walihusika katika makosa yaliyochangia kufutwa
kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agosti.
Uchaguzi mpya utafanyika tarehe 26 Oktoba
lakini Nasa wanasema sharti mabadiliko yafanyike kwenye tume hiyo kabla yao kukubali kushiriki katika
uchaguzi huo.
WAFUASI WA UPINZANI NCHINI KENYA WAENDELEA KUANDAMANA
Reviewed by safina radio
on
October 02, 2017
Rating:

No comments