RAIS WA TANZANIA MH. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAJUMBE WA SERIKALI ZA MITAA ALAT

TAREHE 03-10-2017

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MH. JOHN MAGUFULI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Magufuli amewataka wajumbe wa Jumuiya inayounganisha serikali za mitaa nchini ALAT kuungana kwa pamoja kudhibiti mianya inayopoteza mapato yanayotokana na raslimali za nchi ili kuwanufaisha wananchi wa hali ya chini pamoja na nchi kwa ujmla.

Rais Magufuli ametoa wito huo leo katika mkutano mkuu wa ALAT uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julias Nyerere jijini Dar es salaam ambapo amesema adui wa maendeleo ni kukosa umoja na kuendekeza rushwa na ubadhirifu wa mali unaofanywa na baadhi ya watu wasio waaminifu.

Aidha Dk Magufuli ameeleza kuwa Tanzania imekuwa ikipoteza kiasi kikubwa cha kodi kutokana ubebaji holela wa madini na usainishwaji wa mikataba inayofanywa na baadhi ya watu na makampuni yanayojishughulisha na uchimbaji huo wa madini nakusema kuwa tangu madini aina ya Tanzanite yaanze kuchimbwa Tanzania imepata asilimia tano ya mapato ya madini hayo.


Licha ya hayo Rais Magufuli ameeleza kuwa Serikali imepiga hatua kubwa katika miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi hususani katika nyanja za elimu,miundombinu ya barabara, afya, ikiwemo uagizaji wa madawa na vifaa tiba kutoka viwandani, maji ambapo kumezinduliwa ya miradi ya maji katika halmashauri za miji na vijijini katika mikoa mbalimbali hapa  nchini.
RAIS WA TANZANIA MH. MAGUFULI AFUNGUA MKUTANO WA 33 WA WAJUMBE WA SERIKALI ZA MITAA ALAT RAIS WA TANZANIA  MH. MAGUFULI  AFUNGUA  MKUTANO  WA 33 WA  WAJUMBE  WA  SERIKALI  ZA  MITAA  ALAT Reviewed by safina radio on October 03, 2017 Rating: 5

No comments