IGP SIMON SIRRO AWATAKA WANASASIASA KUACHA KUINGILIA MAJUKUMU YA JESHI LA POLISI
TAREHE 06-10-2017
Mkuu wa jeshi la polisi
nchini IGP Simon Sirro amewataka wanasiasa kuacha kuingilia majukumu ya Jeshi
la polisi juu ya upelelezi wa watuhumiwa wa shambulio la mbunge wa Singida
Mashariki Mh. Tundu Antipasi Lissu.
IGP Sirro ametoa kauli
hiyo Mkoani Njombe kufuatia kuwepo kwa baadhi ya Wabunge kukosoa kauli yake
aliyoitoa akiwa mkoani Mtwara ya kumtaka dereva wa Mbunge huyo kuripoti kwa ajili
ya kutoa taarifa kuhusu upelelezi wa tukio la kujeruhiwa kwa Mbunge huyo.
Amesema kuwa Jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili
kupata ushahidi unaojitosheleza na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano ili
kurahisisha upatikanaji wa taarifa hizo.
Aidha katika hatua
nyingine, IGP Sirro amesema njia ya kumaliza mauaji yanayohusishwa na imani za
kishirikina ni elimu kutolewa kwa wananchi kuupitia vyombo vya habari na nyumba
za ibada kutokana na kuripotiwa kwa vitendo vya kiuhalifu vinavyohusishwa na
imani za kishirikina, visasi na ubakaji
mkoani Njombe.
IGP SIMON SIRRO AWATAKA WANASASIASA KUACHA KUINGILIA MAJUKUMU YA JESHI LA POLISI
Reviewed by safina radio
on
October 06, 2017
Rating:

No comments